Sheria za Matumizi

Utangulizi

Karibu Jumia Deals.co.tz. Kwa kufikia Jumia Deals.co.tz na tovuti, huduma, programu-tumizi au zana zake husiani (Kwa pamoja zinarejelewa kama "Jumia Deals.co.tz") unakubaliana na sheria zifuatazo, ikijumuisha zile zinazopatikana kwa vingo, ambazo zimeundwa ili kuhakikisha kwamba Jumia Deals.co.tz inafanya kazi kwa kila mtu. Jumia Deals.co.tz imetolewa kwako na RS-C Internet Services Company Limited. Sheria hizi za Matumizi zinajumuisha makubaliano yanayofunga kisheria kati yako na Jumia Deals.co.tz kuanzia Februari 2015 kwa watumizi wa sasa, na baada ya kuwakubali watumizi wapya. Unakubali Sheria hizi za Matumizi kwa kubofya kitufe cha "Unda Akaunti" unaposajili akaunti ya Jumia Deals.co.tz na kwa vinginevyo kufikia au kutumia tovuti, huduma, programu-tumizi na zana za Jumia Deals.co.tz; au kama ilivyoelezewa vinginevyo kwenye tovuti, huduma, programu-tumizi au zana maalum.

Utumiaji wa Jumia Deals.co.tz

Kama sharti la matumizi yako ya Jumia Deals.co.tz (ikijumuisha Jumia Deals.co.tz na tovuti, huduma, programu-tumizi na zana zake husiani) unakubaliana kwamba: hautakiuka sheria zozote; hautakiuka Kanuni za Uchapishaji; hautaweka nyenzo yoyote yenye vitisho, matusi, kukashifu au uchafu; hautaweka au vinginevyo kuwasiliana nyenzo yoyote ya uongo au kupotosha au ujumbe wa aina yoyote, hautakiuka haki ya comvo chochote kingine; hautasambaza taka, barua mnyororo, au kukuza miradi ya piramidi; hautasambaza virusi au teknolojia nyingine zozote zinazoweza kudhuru Jumia Deals.co.tz au maslahi au mali ya watumizi wa Jumia Deals.co.tz; hautalazimisha au kuchangia katika kulazimisha mzigo usio na maana katika miundombinu yetu au kuingilia ufanyikazi sahihi wa Jumia Deals.co.tz; hautanakili, kurekebisha, au kusambaza maudhui ya mtu mwingine yeyote bila ridhaa yao; hautatumia buibui robot yoyote, mpapuro au njia nyingine otomati kufikia Jumia Deals.co.tz na kukusanya maudhui kwa madhumuni yoyote bila ruhusa yetu ya moja kwa moja kwa maandishi; hautavuna au vinginevyo kukusanya taarifa kuhusu wengine, ikijumuisha anwani za barua pepe, bila ridhaa zao; hautanakili, kurekebisha wala kusambaza haki au maudhui kutoka tovuti, huduma, programu-tumizi au zana za Jumia Deals.co.tz au haki miliki na alama za biashara za Jumia Deals.co.tz, hautavuna au vinginevyo kukusanya taarifa kuhusu watumizi, ikijumuisha anwani za barua pepe, bila ridhaa zao; hautaruka bypass hatua zinazotumiwa kuzuia au kuwekea vikwazo ufikiaji wa Jumia Deals.co.tz; hautauza vitu yoyote bandia au vinginevyo kukiuka hati miliki, biashara au haki nyingine za vyombo vingine. Unawajibika peke yako kwa taarifa yote unayowasilisha kwa Jumia Deals.co.tz na matokeo yoyote ambayo huenda yakatokana na uchapishaji wako. Tunahifadhi haki kwa hiari yetu ya kukataa au kufuta maudhui tunayoamini sio sahihi au yanakiuka sheria zilizohapo juu. Pia tunahifadhi haki kwa hiari yetu ya kuwekea vikwazo utumizi wa mtumizi wa Jumia Deals.com iwe kwa muda tu au kabisa, au kukataa usajili wa mtumizi. Tukiamini kuwa unakiuka maadili ya Sheria hizi za Utumizi kwa njia yoyote na/au unaonekana mwenye tuhuma kwenye tovuti, huduma, programu-tumizi au zana za Jumia Deals.co.tz, tunaweza, kwa hiari yetu, kuwajulisha watumizi wengine wa Jumia Deals.co.tz ambao wamewasiliana nawe na kupendekeza kwamba wawe waangalifu.

Utumiaji mbaya wa Jumia Deals.co.tz

Jumia Deals.co.tz na jamii yake zinafanya kazi pamoja ili kuweka tovuti, huduma, programu-tumizi na zana za Jumia Deals.co.tz zikiwa zinafanya kazi vizuri na kuweka jamii salama. Tafadhali ripoti kwetu matatizo, maudhui ya kukera na ukiukaji wa sera kwa kutumia mfumo wa kuripoti. Bila kuwekea kikwazo suluhu nyingine, huenda tukatoa onyo, kikomesha au kusitisha huduma yetu, kuondoa maudhui yaliyowekwa na kuchukua hatua za kiufundi na za kisheria ili kuweka watumizi nje ya Jumia Deals.co.tz tukifikiri kwamba wanatengeneza matatizo, wanakiuka haki za vyombo vingine au kutenda sambamba na maana au lengo la sera zetu (ikijumuisha, bila vikwazo, kusimamishwa kwa muda au kabisa au kuwasumbua waajiriwa au watumizi wengine wa Jumia Deals.co.tz). Hata hivyo, iwe tuamue kuchukua yoyote ya hatua hizi, kuondoa maudhui yaliyowekwa au kumuondoa mtumizi nje ya Jumia Deals.co.tz au la, hatuna wajibu wowote wa kufuatilia taarifa zilizowasilishwa au kuhifadhiwa katika tovuti, huduma, programu-tumizi na zana zetu na hatukubali dhima yoyote kwa maudhui bila idhini au kinyume cha sheria kwenye Jumia Deals.co.tz au utumizi wa Jumia Deals.co.tz na watumizi.

Soko la Kiulimwengu

Baadhi ya vipengele vya Jumia Deals.co.tz zinaweza kuonyesha tangazo lako kwenye tovuti, huduma, programu-tumizi na zana zingine ambazo ni sehemu ya jamii. ya kimataifa ya Jumia Deals.co.tz. Kwa kutumia Jumia Deals.co.tz, unakubaliana kwamba matangazo yako yanaweza kuonyeshwa kwenye tovuti, huduma, programu-tumizi na zana hizi zingine. Sheria za tovuti, huduma, programu-tumizi na zana zetu zingine ni sawa na sheria hizi, lakini unaweza kuwa chini ya sheria za ziada au vikwazo vingine katika nchi ambapo tangazo lako limewekwa. Unapochagua kuweka tangazo lako kwenye tovuti, huduma, programu-tumizi au zana nyingine, unaweza kuwajibika kwa kuhakikisha kwamba halikiuka tovuti, huduma, programu-tumizi na zana nyingine kama ile. Huenda tukaondoa tangazo lako ikiwa limeripotiwa kwenye tovuti, huduma, programu-tumizi au zana zetu zingine, au ikiwa tunaamini linasababisha matatizo au linakiuka sheria au sera yoyote.

Maudhui

Jumia Deals.co.tz ina maudhui inayotolewa na sisi, wewe, na watumizi wengine. Jumia Deals.co.tz ni inalindwa na sheria za hakimiliki na mikataba ya kimataifa. Maudhui yaliyoonyeshwa kwenye au kupitia Jumia Deals.co.tz yanalindwa kama kazi kwa pamoja na/au mkusanyiko, kulingana na sheria za hakimiliki na mikataba ya kimataifa. Unakubaliana kutonakili, kusambaza au kurekebisha maudhui kutoka Jumia Deals.co.tz bila ya ridhaa yetu ya moja kwa moja kwa maandishi. Hauwezi kutoanisha au kutenganisha, kuhandisi kinyume au vinginevyo kujaribu kugundua msimbo asili ulioko katika katika Jumia Deals.co.tz. Bila kuwekea vikwazo yaliyotajwa, unakubaliana kutozalisha, kunakili, kuuza, kuuza tena, au kutumia kwa madhumuni yoyote kipengele chochote cha Jumia Deals.co.tz (isipokua maudhui yako mwenyewe). Unapotupea maudhui, unatupa na kuwakilisha kwamba una haki ya kutupa, haki isiyo ya kipekee, ya kiulimwengu, ya milele, isiyo batilika, bila mrabaha, inayoweza kutolwa leseni zingine ndogo (kupitia nyanja mbalimbali) ya kutumia hakimiliki yoyote na zote, utangazaji, alama za biashara, muundo, hifadhidata na hakimiliki za mali ya kitaaluma kwa maudhui hayo, katika mfumo wowote unaojulikana sasa kujua au utakaugunduliwa siku zijazo na kwenye tovuti, huduma, programu-tumizi na zananyingine zote ambazo ni sehemu ya jamii ya kimataifa ya Jumia Deals.co.tz, kama vile Jumia Deals.co.tz au tovuti zetu za matangazo maalum katika nchi zingine. Kwa ziada, unasalimisha haki zote ulizonazo katika maudhui hayo kwa uenezi kamili zaidi unaoruhusiwa na sheria.

Ukiukaji

Usichapishe maudhui ambayo yanakiuka haki za vyombo vingine. Hii inajumuisha, lakini si tu, maudhui ambayo yanakiuka haki za mali ya kitaaluma kama vile hakimiliki, muundo na alama ya biashara (k.m. kutoa vitu bandia kwa mauzo). Idadi kubwa ya bidhaa za aina zote zinazotolewa kwenye Jumia Deals.co.tz na watu binafsi. Vyombo vyenye haki, haswa wamiliki hakimiliki, haki za alama za biashara au haki nyingine wanaweza kuripoti tangazo lolote ambalo huenda likakiuka haki zao, na kuwasilisha ombi tangazo kama lile kuondolewa. Mwakilishi wa kisheria wa chombo chenye haki katika njia sahihi, bidhaa zinazokiuka haki za mali ya kitaaluma zitaondolewa na Jumia Deals.co.tz.

Kuripoti ukiukaji:

Ili kushiriki katika mpango wa Ilani ya Ukiukaji, unahitaji tu kukamilisha Fomu ya Ilani ya Ukiukaji na ulitume kwa barua pepe kwa Jumia Deals.co.tz: [email protected] Unaweza kutumia fomu hii, kamili na sahihi yako, kuripoti matangazo ambayo huenda yakakiuka haki za mali yako. Taarifa iliyoagizwa katika Fomu ya Ilani ya Ukiukaji ni ya dhumuni la kuhakikisha kwamba vyombo vinavyoripoti vipengee hivi ni aitha chombo chenye haki au waakilishi wao wenye idhini rasmi. Habari hii ni lazima pia iwezeshe Jumia Deals.co.tz kutambua tangazo lakuondolewa. Mara tu tumepokea Fomu yako ya Ilani ya Ukiukaji iliyojazwa sahihi, unaweza kuituma kwa urahisi baadaye kwa Jumia Deals.co.tz kwa kupitia anuani iliyotolewa ya barua pepe. KUMBUKA: FOMU HII INAWEZA TU KUTUMIWA NA WAMILIKI HALALI WA HAKI HUSIKA ZA MALI YA KITAALUMA. "ILANI YA UKIUKAJI" IMEKUSUDIWA KUWAWEZESHA WAMILIKI HAKI KUHAKIKISHA KWAMBA BIDHAA ZINAZOTOLEWA NA WATUMIZI WA VENDITO.COM HAZIKIUKI HAKIMILIKI ZAO, ALAMA ZA BIASHARA AU HAKI NYINGINE ZA MALI YA KITAALUMA.

Dhima

Hakuna chochote katika sheria hizi zitawekea dhima yetu vikwazo kwa uwakilishi mbaya wa kiulaghai, au kwa kifo au jeraha la kibinafsi kutokana na utelekezaji wetu au utelekezaji wa mawakala au waajiriwa wetu. Unakubaliana kutotuchukua kama wanaowajibika kwa mambo watumizi wengine wanayochapisha au kufanya. Huwa tunapitia machapisho ya watumizi lakini hatuhusiki katika shughuli halisi za kati ya watumizi. Kwa kuwa maudhui mengi kwenye Jumia Deals.co.tz huja kutoka kwa watumizi wengine, hatuhakikishii usahihi wa machapisho au mawasiliano ya watumizi au ubora, usalama, au uhalali wa kinachotolewa. Hakuna wakati tunakubali dhima ya maelezo yoyote kwa uchapishaji wa taarifa isio halali, inayotisha, yenye matusi, ya kukashifu au chafu, au nyenzo ya aina yoyote inayokiuka haki za mtu yeyote mwingine, ikijumuisha bila vikwazo wasilisho zozote inayohusu au inayotia moyo tabia inayoweza kuhusu kosa la jinai, kuibua dhima ya kiserikali au vinginevyo inakiuka sheria yoyote husika. Unakiri kwamba hatuwezi kuthibitisha ufikiaji endelevu, bila hitilafu au salama kwa huduma zetu au kwamba kasoro katika huduma zitarekebishwa. Huku sisi tutatumia juhudi nzuri ili kudumisha huduma bila hitilafu, hatuwezi kuthibitisha hili na hatuwezi kutoa ahadi zozote au dhamana (iwe moja kwa moja au husiani) kuhusu uendeshaji na upatikanaji wa tovutiu, huduma, programu-tumizi au zana zetu. Vifaavyo, kwa uenezi unaoruhusiwa kisheria inaruhusiwa tunajiondoa moja kwa moja kutoka kwa dhamana zote, uwakilishi na masharti, moja kwa moja au husiani, ikijumuisha yale ya ubora, uuzaji, ubora wa uuzaji, uimara, uzima kwa dhumuni fulani na yale yanayotokana na amri. Hatuwajibiki kwa hasara yoyote, iwe ya fedha (ikijumuisha faida), ukarimu, au sifa, au yoyote maalum, isio ya moja kwa moja, au madhara yoyote yanayotokana na utumizi wako wa, au kutoweza kutumia Jumia Deals.co.tz, hata utushauri au tungeweza kutabiri uwezekano wa hasara yoyote kama ile kutokea. Mamlaka nyingine haziruhusu kujiondoa kutoka kwa dhamana au uchapishaji kando hasara, kwa hivyo kujiondoa kama kule kutoka kwa lawama na uchapishaji kando huenda kusitumike kwako. Licha ya aya ya awali, tukipatikana kuwa tunawajibika, dhima yetu kwako au chombo kingine (iwe katika mkataba, ukiukaji, utelekezaji, dhima kali katika ukiukaji, kwa amri au vinginevyo) ina mpaka kwa pakubwa zaidi ya (a) ada jumla unatulipa kwetu katika kipindi cha miezi 12 kabla ya hatua inayoibua dhima, na (b) 100 (Sarafu ya ndani)

Kuondoa

Ikiwa una mgogoro na mtumizi moja au zaidi wa Jumia Deals.co.tz, unatuondoa (na maafisa, wakurugenzi, mawakala, matawi, ubia na wafanyakazi wetu) kutoka kwa madai, mahitaji na hasara zozote (halisi na yakusababishwa) za kila aina na hali, zinazojulikana au hazijulikani, zinazoibuka kutokana na au kuhusiana na migogoro kama ile.

Taarifa ya Kibinafsi

Kwa kutumia Jumia Deals.co.tz, unakubaliana na ukusanyaji, uhamisho, uhifadhi na utumizi ya taarifa yako ya kibinafsi na Jumia Deals.co.tz kwenye seva zilizoko Ulaya au sehemu nyingine yoyote, Kama ilivyoelezewa zaidi katika Sera yetu ya Faragha. Unakubaliana pia kupokea mawasiliano ya uuzaji kutoka kwetu isipokuwa utueleze kwamba haungependa kupokea mawasiliano kama yale.

Suluhu kwa migogoro

Mgogoro ukiibuka kati yako na Jumia Deals.co.tz, tunakuhimiza kwa nguvu kwanza uwasiliane nasi moja kwa moja ili kutafuta suluhisho la kwa kwenda kwa Jumia Deals.co.tz Ukurasa wa usaidizi.Tutazingatia maombi ya busara ya kutatua mgogoro kwa taratibu mbadala wa kusuluhisha mgogoro, kama vile upatanishi au usuluhishi au mbadala kwa madai.

Jumla

Hizi sheria na sera nyingine zilzochapishwa kwenye Jumia Deals.co.tz zinajumuisha makubaliano kamili kati ya Jumia Deals.co.tz na wewe, ikiwa na nguvu kuliko makubaliano yoyote ya awali. Hakuna shirika, ushirikiano, ubia, uhusiano wa mfanyakazi-mwajiri au mtoa leseni-mpokea leseni unakusudiwa au kuundwa na kubaliano hili.

Kubaliano hili litaongozwa na kufafanuliwa katika uzingatiaji wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Unakubaliana kwamba dai au mgogoro wowote unaoweza kuwa nao dhidi ya Jumia Deals.co.tz lazima utatuliwe na mahakama za YANGON ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wewe na Jumia Deals.co.tz mnakubaliana kunyenyekea kwa mamlaka ya kipekee ya mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukikosa kutekeleza kifungu chochote fulani, hatuondoi haki yetu ya kufanya hivyo baadaye. Mahakama ikipiga kalamu yoyote ya sheria hizi, sheria zinazosalia zinaendelea kutawala. Tunaweza kutoa kubaliano hili kiotomati kwa hiari yetu pekee kulingana na kifungu cha ilani hapo chini.

Ila kwa ilani zinazohusiana na maudhui haramu au kiukaji, ilani zako kwetu lazima zitumwa kwa barua pepe iliyosajiliwa kwa [email protected] Tutatuma ilani kwako kupitia anwani ya barua pepe unayotoa, au kwa anuani ya posta iliyosajiliwa. Ilani zilizotumwa kwa banuani ya posta iliyosajiliwa itachukuliwa kupokewa siku tano baada ya tarehe ya kutumwa. Huenda tukasasisha kubaliano hili kwa wakati wowote, na sasisho kuchukua usukani wakati unachapisha tena au siku 30 baada ya sisi kuchapisha sera iliyosasishwa kwenye tovuti ya Jumia Deals.co.tz, yoyote inayotangulia. Hakuna marekebisho mengine kwa makubaliano haya yatachukua usukani isipokuwa yamefanywa kwa maandishi, na kutiwa sahihi na watumizi na nasi.

Kwa usaidizi wowote kutumia Jumia Deals.co.tz tafadhali tembelea tovuti ya Jumia Deals.co.tz Ukurasa wa Usaidizi.